MATENGENEZO
Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro una hanga la ukubwa wa 110 x 83 Sqm na urefu wa Mita 23 (kwenda juu), Hanga hilo likiwa na uwezo wa kuhifadhi ndege kubwa aina ya Boeng 747 au MD11 au ndege mbili aina ya ATR kwa wakati mmoja. Uwepo wa hanga hilo lenye vifaa unafanya shughuri za matengenezo kuwa rahisi zaidi kwani huduma mbalimbali za ufundi hufanyika kiwanjani hapo kwa urahisi. Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro unakuwa miongoni mwa viwanja vichache vya ndege barani Afrika vyenye hanga kubwa zaidi.

