Fursa za Biashara
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro upo kandokando ya barabara ya Moshi-Arusha ukiwa na ukubwa wa kilomita za maraba 110. Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro umeedelea kuwa ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutoa huduma bora za usafiri wa anga na shughuri zingine zifananazo. Zaidi ya abiria milioni moja (1,000,000) hutumia uwanja huu kila mwaka. Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro unazaidi za mita za mraba 350 zenye maduka na sehemu za kufanya manunuzi, mita za mraba 330 za eneo la mizigo pamoja na eneo kubwa la uendeshaji wa shughuri za mafuta ya ndege.
Ukiona fursa yeyote ya biashara katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro tafadhari fika ofisi za mamlaka ya uwanja au piga simu +255(0)272554252 au +255(0)272554252.

