emblem

Kilimanjaro International Airport
KADCO

KADCO Logo

ZIMA MOTO & UOKOAJI

Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro unahuduma ya zima moto na uokoaji kwa muda wote (Masaa 24). Uwanja una vifaa vya kisasa vya kuzimia moto na vile vya huduma za dharula, ambapo timu hii ya uokoaji hukaa karibu kabisa na eneo la kutualia pamoja na lile la maegesho ya ndege. Huduma za zimamoto na uokoaji katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro umepewa daraja la 9 (tisa) kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Usimamizi wa Anga (ICAO). Wataalamu pamoja na vifaa vya zima moto na uokoaji hufanyiwa ukaguzi mara kwa mara ili kuendana na mabailiko na mahitaji ya huduma huduma husika.