Usafiri
Huduma za Usafiri wa Magari
Huduma za Teksii
Huduma za teksii katika Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro ni wa haraka na uhakika. Huduma hizi zinapatika hatua chache kutoka lango kuu la kuwasili abiria kuelekea kokote kule ndani ya jiji la Arusha, Moshi na ukanda wote wa Kaskazini. Madereva wa huduma hizi ni marafiki na ni watu wanaojua maana harisi ya kujali kazi zao na muda pia.
Kuendesha gari lako binafsi
Kama wewe ni mwenyeji katika barabara za mkoa huu, bila shaka inakupa fursa ya kuendesha gari yako mwenyewe. Hii yote inachagizwa na urahisi wa kupata sehemu ya kupaki magari, urahisi wa kupata tiketi ya maegesho ya magari, gharama ndogo za maegesho ya magari, pia kutokuwepo na foleni.
Usafiri wa Umma (Share rides)
Gharama za huduma hii ni kuanzia Tsh 10,000 tu ambapo wewe na abiria wengine mnaoelekea uelekeo mmoja mtachangia chombo cha usafiri kutoka uwanja wa ndege wa kilimanjaro kuelekea Arusha au Moshi. Huduma hii ni ya gharama nafuu pia inakupa fursa ya kufurahia safari mkiwa pamoja na wasafiri wengine. passengers

